Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Mara

DKT. GRACE MAGEMBE AHIMIZA UTOAJI HUDUMA BORA KWA WANANCHI KWA KUZINGATIA WELEDI NA MAADILI

Posted on: February 21st, 2024


Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere – Mara wahimizwa kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia weledi na maadili.

Hayo yamesemwa leo na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara, Dkt. Grace Magembe amesema kuwa watumishi wa afya wanatakiwa kuwahudumia wananchi kwa kuzingatia weledi na maadili ili kuepuka kupelekwa kwenye mabaraza ya kinidhamu.

Aidha Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dkt. Osimund Dyegura amemshukuru Naibu katibu Mkuu Dkt. Grace Magembe kwa ziara hiyo na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Katika ukaguzi huo Dkt. Grace Magembe alipita maeneo mbalimbali na kuangalia namna huduma zinavyotolewa kwa wananchi na kutoa pongezi katika maeneo aliyopita ambayo ni Idara ya kinywa na meno pamoja na Wodi la watoto wachanga.